ukome kunifamia, sipati wako wasaa,
bokisi sitaingia, katakata nakataa,
hadharani nakwambia, hakuna wa kukufaa,
pumbavu nakwambilia, kwangu wewe ni balaa,
mafuta wajipakia, kwenye rangi ya makaa,
ndo wengi kuwavutia, njiani na kwenye baa,
sasa doa una mia, usoni umefukaa,
pumbavu nakwambilia, kwangu wewe ni balaa,
tembo unafurahia, chang'aa pia busaa,
huku wajindanganyia, mwili utachanjamaa,
hakika utajutia, akili ukipagaa,
pumbavu nakwambilia, kwangu wewe ni balaa,
nashindwa kufikiria, siketi unazovaa,
mapaja 'mefichulia, ni lini utakomaa,
uweze kuyafichia, ghulamu wenye tamaa,
pumbavu nakwambilia, kwangu wewe ni balaa,
miguu wapanulia, vijana bila janaa,
bila kujihurumia, kodomu unakataa,
huku wajindanganyia, vitembe vitakufaa,
pumbavu nakwambilia, kwangu wewe ni balaa,
baba wanakukujia, kutoa zao hawaa,
huku wakishangilia, hakika unatufaa,
pesa zao zafutia, je na gonjwa la zinaa?
pumbavu nakwambilia, kwangu wewe ni balaa,
mwishoni nimefikia, mali yangu napagaa,
nadhani umesikia, banati mwenye kichaa,
sioni ikifikia, nipate wako wasaa,
pumbavu nakwambilia, kwangu wewe ni balaa,
SHUKRANI.
Marc Karash - 0707090505

No comments:
Post a Comment