MAMA
Mama yangu shika kiti, nikupe kongole zangu,
Mama rafiki wa dhati, fundi wa maisha yangu,
Mama kila wakati, ulijali maishangu,
Mama ulinipa kuti, pokea kongole zangu,
Mama hukunifeliti, katika unyonge wangu,
Mama ulijizatiti, kamasi kutoa pangu,
Mama aidha upati, ulifunga uchi wangu,
Mama ulinipa kuti, pokea kongole zangu,
Mama hukunisaliti, hukunijaza uchungu,
Mama ulinipa titi, katika uchanga wangu,
Mama 'linipa jaketi, baridi ikija kwangu,
Mama ulinipa kuti, pokea kongole zangu,
Mama 'kifanya bajeti, hukosi viguo vyangu,
Mama hukosina juti, kukinga viguu vyangu,
Mama hukosi tendeti, kushibisha tumbo langu,
Mama ulinipa kuti, pokea kongole zangu,
Mama yu mwinjilisti, wa dini rohoni mwangu,
Mama nikawa tisti, katika imani yangu,
Mama niko na tiketi, ya kuingia kwa Mungu,
Mama ulinipa kuti, pokea kongole zangu,
Mama ukiwa hayati, utoke machoni pangu,
Mama yako hasanati, 'tahisi moyoni mwangu,
Mama nikifunga beti, nakupa kongole zangu,
Mama ulinipa kuti, pokea kongole zangu,
Shukrani- malenga Marc Karash
Thursday, 1 March 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HADITHI YA KUSISIMUA
ANN NA MUTUVIE Jina lake ni Ann. Sura anayo ndio, umbo analo ndio pia tabasamu lake lingemvutia kila mtu kwenye gari waliyoisafiri. M...
-
MAMA Mama yangu shika kiti, nikupe kongole zangu, Mama rafiki wa dhati, fundi wa maisha yangu, Mama kila wakati, ulijali maishangu, Mama...
-
MPENZI WANGU Tangu nilipokuona, ninahisi nina deni, Kuna jambo sijanena, laninyima burudani, Najaribu kulinena, sasa mara elfeni,...
-
MATHAYO 5 : 14 -16 Jukumu ninajitwika, kushukuru wetu mu’mba, Kutuwezesha kufika, kwenye takatifu jumba, Nadhani ninasikika, nany...
No comments:
Post a Comment