usinipite njiani, kwa gari bila salamu,
uniache kwa huzuni, aidha nikilaumu,
na kushindwa ni kwa nini, sahibu huniheshimu,
usione kuwa chini, kama ni yangu rajamu,
kunaye yule razini, hivi leo ni timamu,
wanafunzi wa shuleni, wamekuwa waalimu,
chokora wa mitaani, wameandaa karamu,
usione kuwa chini, kama ni yangu rajamu,
usinite masikini, nikibibu yako simu,
usiseme akilini, hana kauli muhimu,
labda u hatarini, nakuepusha na bomu,
usione kuwa chini, kama ni yangu rajamu,
yule mwizi wa samani, hivi leo ni hakimu,
yule zuzu wa zamani, hivi leo ni alimu,
Halima Mama Madeni, analipa tasilimu,
usione kuwa chini, kama ni yangu rajamu
,
nikija kwako kazini, nisiwe najaza fomu,
na nisitoshwe faini, kukosa kukuheshimu,
nissiitwe mhaini, nikikataa haramu,
usione kuwa chini, kama ni yangu rajamu,
kalamu naweka chini, hata kama kwa ugumu,
ni leo tu niko chini, ninataka ufahamu,
kesho niwe kileleni, nikila matunda tamu,
usione kuwa chini, kama ni yangu rajamu,
SHUKURANI
MARC KARASH 0707090505

No comments:
Post a Comment