Thursday, 1 March 2018

BARUA KWA ONINGA
Nakwandikia barua, mheshimiwa oninga,
nadhani unatambua, pingu ulizoifunga,
kenya kama jumuia, na kisha kuibananga,
Najua ninachojua, na tena twakubiringa,


Usituone kimia, Ukadhani ni ujinga,
Hatua twakwesabia,Tukutie kwenye tenga,
Macho hutaaminia,Wakifumka wajinga,
Najua ninachojua, na tena twakubiringa,

Huwezi ukachelea, Kushtua vifaranga,
Wanaojikazania, Na kuishi kujipanga,
Mtihani kukalia, Za shule wavue kanga,
Najua ninachojua, na tena twakubiringa,

Nchi umeichafua, Kwa tendawili na genga,
Hoja tukifikiria, Unasimama kupinga,
Unachokikazania, Mwishowe kitakunonga,
Najua ninachojua, na tena twakubiringa,

Saka wa kukuongoa, Sabu tunakuchabanga,
Kisiasa twakuua, Na tuje kwenye matanga,
Boma lako tia ua, Na utengeze ufinga,
Najua ninachojua, na tena twakubiringa,

Hivi sasa natulia, Na beti ninazifunga,
Baba nakushauria, Usakane na wahenga,
Waweze kukuelezea, Lipi nililolifunga,
Najua ninachojua, na tena twakubiringa,

SHuKRANI - Malenga MarcKarash.

No comments:

Post a Comment

HADITHI YA KUSISIMUA

ANN NA MUTUVIE Jina lake ni Ann. Sura anayo ndio, umbo analo ndio pia tabasamu lake lingemvutia kila mtu kwenye gari waliyoisafiri. M...